Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza mara
baada ya kukagua ujenzi wa mabweni katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
..........................................................................................
Na:
Lilian Lundo - MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 7 kwa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kulipa deni la bilioni 2 ambalo wanadaiwa na Shirika
la nyumba la Taifa (NHC).
Dkt. Magufuli ametoa agizo
hilo kwa Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Injinia Joseph Nyamhanga leo jijini
Dar es Salaam katika ziara ya kushtukiza ya kuangalia ujenzi wa hosteli za
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
“Nawapa siku 7 muwe mmelilipa
hilo deni huku mkiendelea na utaratibu wa kuhamia Dodoma, kama hamtalilipa kwa
wakati nitawaagiza NHC kuwatolea vitu vyenu nje kama wanavyofanya kwa wengine,”
alisema Dkt. Magufuli.
Amesema kuwa kiwango
hicho cha bilioni 2 kingeiwezesha wizara hiyo kujenga ofisi za wizara kwa kuwatumia
Wakala wa Majengo (TBA) ambao wako chini ya wizara hiyo badala ya kutumika kama
kodi ya
pango.
pango.
Aidha, ameitaka wizara hiyo
kuhamia Mjini Dodoma mara tu watakapokamilisha deni hilo na kutoendelea kupanga
jijini Dar es Salaam, kwani hakuna sababu ya kuendelea kupanga majengo ya ofisi
Dar es Salaam wakati Serikali yote inahamia Dodoma.
Wakati huohuo, Rais
Dkt. Magufuli ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Tecknolojia, Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Wakala wa Majengo (TBA) na uongozi wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam kwa kusimamia vizuri mradi wa ujenzi wa hosteli za chuo
kikuu ambao Rais mwenyewe aliahidi shilingi bilioni 10 katika ujenzi huo,
bilioni 5 imekwishatolewa na bilioni nyingine 5 itatolewa ndani ya wiki hii.
Hosteli hizo
zinategemea kuchukua wanafunzi 4000 ambapo itapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo
la wanafunzi kukaa nje ya maeneo ya chuo.

0 Comments