Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt. Medard Kalemani akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao
cha pili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
Na
Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.
Mikoa
ya Lindi na Mtwara itaondokana na hali ya kukatika umeme mara kwa mara katika
maeneo ya Mikoa hiyo inayotokana na ubovu wa Genereta moja kati ya Tisa katika
kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia Gesi Asilia Mtwara.
Hilo
limebainishwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt.
Medard Kalemani alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Newala Mjini Mhe. Kepteni
Mstaafu George Huruma Mkuchika lililouliza “Serikali iliwaahidi wananchi wa
Mikoa ya Lindi na Mtwara umeme wa uhakika na wa kutosha baada ya kugundulika
kwa Gesi lakini bado kumekuwa na tatizo la kukatika kwa umeme?.
Mhe.
Dkt. Medard Kalemani ameeleza kuwa katika kuondokana na tatizo hilo Serikali
inafanya ukarabati wa Mtambo ulioharibika ili kurudisha uwezo wa kituo katika
hali yake ya kawaida ya kuzalisha MW 18.
“
Nia ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma ya Umeme kwa asilimia
kubwa hasa kwa wale waishio vijijini” alisisitiza Mhe. Kalemani.
Ameongeza
kuwa katika kuendeleza juhudi za upatikanaji wa umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara
imeongezewa mitambo sita (6) yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa jumla ya MW 12
kama hatua ya muda mfupi.
Aidha
katika kuboresha hali ya upatikanaji endelevu wa umeme katika Mikoa hiyo,
TANESCO inajenga njia ya kusafirishia umeme yenye msongo wa kilovoti 132 yenye
urefu wa kilomita 80 kutoka Mtwara hadi Mnazi mmoja Lindi.

0 Comments