Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi
Gerson Lwenge akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika akijibu hoja mbalimbali
za wabunge katika kikao cha pili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini
Dodoma.
Na
Raymond Muahumbusi WHUSM Dodoma.
Serikali
kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri
ya Watu wa China, Benki ya Maendeleo ya Waarabu(BADEA),Washirka wa Maendeleo
(DPS), na Serikali ya India kwa pamoja
wametoa jumla ya Shillingi Billion 164 kawa ajili ya kutekeleza mradi wa maji
Chalinze kwa awamu tatu.
Akijibu
Swali Mbunge wa Chalinze (CCM) Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete lililouliza kuwa
Wakazi wa Chalinze wamekuwa katika sintofahamu ya kukamilka kwa mradi wa maji Chalinze?
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge ameeleza kuwa Serikali ipo
katika utekelezaji wa mradi huo na gharama za utekelzaji wake ni Shillingi
Billioni 23.4 kwa awamu ya kwanza na Shillingi Billioni 53.7 kwa awamu ya pili
ya mradi na kwa awamu ya tatu itagharimu Shillingi Billioni 86.9.
Ameongeza
kuwa kukamilika kwa awamu ya kwanza na utekelezaji umekamilika na kwa awamu ya pili
ya mradi huo jumla ya vijiji 88 vimenufaika na kupeleka hali ya upatikanaji wa
maji katika mji wa Chalinze na Vitongoji vyake kufikia asilimi 88 ya wakazi
wote waishio katika eneo lote linalopitiwa na mtandao wa maji.
“Mradi
upo katika hatua nzuri na umekamilika kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili ipo
katika utekelzeaji na wanachi wameanza kunufaika na mradi huu kwa kupata huduma
ya maji” alisisitiza Mhe. Lwenge.
Pia
ameleza kuwa katika awamu ya pili vijiji 12 vya Mwindu,Visakazi, Lulenge,
tukamisasa,Kinonko, Bwawani, Sinyaulime, Gwata, Ngerengere, Kidugalo, Kambi ya
Kinonko na Sangasanga vitaanza kupata huduma ya maji ifikapo mwishoni mwa mwezi
Aprili mwaka 2017 baada ya kukamilika kwa majaribio ya bomba kuu.
Vijiji
vitatu vya Kwang’andu,kifuleta na Kwaruhombo vitaanza kupata maji mara baada ya
mkandarasi kufanya maboresho ya pampu ambazo zimeonekana hazifanyi kazi kama inavyotakiwa
na mkandarasi huyo ameagizwa kuhakikisha
pampu hizo zinafanya kazi kabla ya Juni
2017.
Aidha
kwa sasa Serikali inatekeleza mradi huu kwa awamu ya tatu ambapo upanuzi wa
mtambo wa kuzalisha maji, ujenzi wa mabomba makuu ya kusafirisha maji (KM 115),
Ujenzi wa mfumo wa manomba ya kusambaza maji(KM 1022), Ujenzi wa matanki
makubwa 19 na ujenzi wa vituo 9 vya kuchotea maji na ujenzi wa vioski 351 vya
kuchotea maji vinatekelzwa.

0 Comments