SHEREHE za Tuzo ya Mchezaji Bora
wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kufanyika Mei 24 mwaka huu
ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.
Kamati Maalum iliyoundwa
kusimamia tuzo hiyo imefanya mabadiliko kiasi kwa kuongeza baadhi ya
tuzo ambazo hazikuwepo msimu uliopita lengo ikiwa ni kuboresha tuzo.
Tuzo zilizoongezwa ni: Tuzo ya
Heshima (ambayo itatolewa kwa mwanasoka nguli wa zamani mwenye historia
nzuri kwa soka la Tanzania).
Nyingine ni: Tuzo ya Kikosi Bora
cha Msimu (Itatolewa kwa wachezaji Bora 11 wa Ligi Kuu (VPL XI
2016/2017) walioteuliwa kutokana na ufanisi wao katika ligi hiyo msimu
huu.
Pia imeongezwa Tuzo ya Mchezaji
Bora mwenye chini ya umri wa miaka 20 (Hii itatolewa kwa wachezaji
waliofanya vizuri katika ligi ya vijana ya timu za Ligi Kuu ya Vodacom.
Tuzo hiyo ya Mchezaji Bora wa
Ligi ya Vijana itajulikana kama Tuzo ya Ismail Khalfan ikiwa ni heshima
ya kumbukumbu ya mchezaji Ismail Khalfan wa Mbao FC aliyefia uwanjani
katika mashindano hayo yaliyofanyika mkoani Kagera.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
limefikiria kutoa tuzo hiyo kama njia mojawapo ya kuonesha kuthamini
kipaji cha mchezaji huyi wakati wa uhai wake.
Kutokana na mabadiliko hayo tuzo
zitakazotolewa katika sherehe hizo pamoja na Tuzo ya Mchezaji Bora wa
Ligi Kuu ya VPL ambayo ndiyo tuzo kuu, pia ni Bingwa wa Ligi Kuu,
Mshindi wa Pili, Mshindi wa Tatu, Mshindi wa Nne na Mfungaji Bora.
Nyingine ni Mchezaji Bora wa Ligi
Kuu, Golikipa Bora, Kocha Bora, Mwamuzi Bora, Mchezaji Bora wa Heshima,
Mchezaji Bia anayechipukia, Goli Bora la Msimu, Mchezaji Bora wa
Kigeni, Mchezaji Bora wa Chini ya Umri wa Miaka 20 na Timu Yenye
Nidhamu.
Tuzo za Bingwa, mshindi wa pili, wa tatu na wa nne na Mfungaji Bora hizi zipo kulingana na msimamo wa ligi ulivyo.
Hata hivyo Mfungaji Bora safari
hii kuna wachezaji wawili wamefungana, hivyo kamati itapitia vigezo
vilivyopo katika Kanuni za kumpata Mfungaji Bora w Ligi Kuu Tanzania
Bara ili kupata mshindi ambaye atatangazwa siku hiyo ukumbini.
Wafuatao wameteuliwa kuwania tuzo hizo kutokana na vigezo mbalimbali:
Mchezaji Bora wa Ligi Kuu
Aishi MANULA – Azam
Simon MSUVA – Yanga
Shiza KICHUYA – Simba
Haruna NIYONZIMA – Yanga
Mohammed HUSSEIN – Simba
(Majina ya wanaowania tuzo
hiyo yalitolewa Jumatano iliyopita na upigaji kura unaendelea
ukiwahusisha Makocha wa timu za Ligi Kuu na Makocha Wasaidizi,Wahariri
wa habari za michezo na Manahodha wa timu za Ligi Kuu, ambapo mwisho wa
kufanya hivyo ni Jumanne Mei 23 mwaka huu).
KIPA BORA
Aishi MANULA – Azam
Owen CHAIMA – Mbeya City
Juma KASEJA – Kagera Sugar
KOCHA BORA
Joseph OMOG – Simba
Mecky MEXIME – Kagera Sugar
Ettiene NDAYIRAGIJE – Mbao
MWAMUZI BORA
Shomari LAWI – Kigoma
Elly SASII – Dar es Salaam
Hance MABENA – Tanga
MCHEZAJI BORA WA KIGENI
Haruna NIYONZIMA – Yanga
Method MWANJALE – Simba
Yusuph NDIKUMANA – Mbao
MCHEZAJI BORA ANAYECHIPUKIA
Mbaraka ABEID – Kagera Sugar
Shaaban IDD – Azam
Mohammed ISSA – Mtibwa
TUZO YA ISMAIL KHALFAN – (U-20)
Shaaban IDD – Azam
Abdalah MASOUD – Azam
Mosses KITAMBI – Simba
TUZO YA HESHIMA
(Atatangazwa aliyeteuliwa siku hiyohiyo ya sherehe za tuzo).
GOLI BORA LA MSIMU
(Tayari yamepatikana mabao bora 10 ambayo yataoneshwa siku hiyo ukumbini ikiwemo lile bora la msimu mzima).
TIMU YENYE NIDHAMU
(Mshindi atatangazwa ukumbini siku hiyo kulingana na vigezo vilivyopo).
WACHEZAJI 11 BORA WA MSIMU – VPL XI 2016/17
(Watatangazwa ukumbini siku hiyo ya sherehe).
Kamati inayohusika na usimamizi
wa tuzo inawaomba wadau wote ambao wameombwa kupiga kura katika Tuzo ya
Mchezaji Bora wafanye hivyo kulingana na fomu walizotumiwa na mchango
wao una thamani kubwa.

0 Comments