Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akimkabidhi Hati za
Umiliki wa nyumba 50 za Watumishi wa Afya kwa Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika uwanja wa michezo
wa Mazaina Chato mkoani Geita.
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akizungumza na
wananchi wa Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera katika uwanja wa Mazaina
Chato mkoani Geita kabla ya kukabidhi Hati za umiliki wa nyumba 50 za
watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation)
katika mikoa hiyo mitatu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na wananchi wa Mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera katika
uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita baada ya Rais Mstaafu wa awamu ya
Tatu Benjamin Mkapa kukabidhi nyumba 50 kwa wizara ya Afya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya
kukabidhi nyumba hizo 50 zitakazotumika katika Sekta ya Afya katika
mikoa ya Kagera, Simiyu na Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wakati
Mbunge wa Chato ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.
Medard Kalemani alipokuwa akihutubia wananchi wa Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara baada ya
kumaliza ziara yake Chato mkoani Geita ambapo alikabidhi nyumba 50
zitakazotumika katika sekta ya afya katika mikoa ya Geita, Simiyu na
Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mama Anna Mkapa.
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akiangalia hotuba
yake kabla ya kuhutubia wananchi mbalimbali katika uwanja wa michezo wa
Mazaina Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia wananchi wakati akiwasili katika uwanja wa Mazaina Chato
mkoani Geita.
Kikundi cha ngoma za asili cha Chato kikitumbuiza katika uwanja wa Mazaina Chato mkoani Geita
Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida akimkabidhi Mkuu wa
Wilaya ya Chato Shaaban Ntarambe hati ya kituo cha kukamua Mafuta ya
Alizeti (Double Refine) kilichojengwa Chato mkoani Geita kwa Msaada wa
Serikali ya Japan.
PICHA NA IKULU















0 Comments