Muwezeshaji wa Semina kuhusu Mfumo Mpya wa
Uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Serikali za Mitaa (PlanRep) Bw. Geofrey
Mackenzi akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo inanyoendele Jijini Mbeya.
Katikati ni Katibu Tawala Msaidizi, Mipango na Uratibu kutoka Mkoa wa Njombe Amza Amen Ndossa na
Muwezeshaji kutoka OR – TAMISEMI Bw. Allan Bendera.
Muwezeshaji kutoka PS3 Bw. John
Machonchoryo akifafanua jambo mbele ya
washiriki wa Semina kuhusu Mfumo Mpya wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti katika
Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini
Mbeya. Katikati ni Katibu Tawala Msaidizi, Mipango na Uratibu kutoka Mkoa wa Njombe Bw. Amza Amen Ndossa na
Muwezeshaji kutoka OR – TAMISEMI Bw. Jeremiah Mtawa.
Muwezeshaji wa masuala ya Tehama Bw. David
Nyangaka akifafanua jambo mbele ya
washiriki wa Semina kuhusu Mfumo Mpya wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti katika
Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini
Mbeya.
Muwezeshaji wa masuala ya Tehama Jeremiah
Mwambange akitoa maelekezo kwa washiriki wa Semina kuhusu Mfumo Mpya wa
Uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini Mbeya.
Baadhi
ya washiriki wa semina kuhusu Mfumo mpya wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti
katika Serikali za Mitaa (PlanRep) wakifuatilia kwa makini mafunzo hay oleo
Jijini Mbeya. Mafunzo hayo yamelenga kuwa jengea uwezo watumiaji wa mfumo huo
katika Halmashauri zote nchini chini ya ufadhili wa USAD Tanzania/PS3
Picha
na: Idara ya Habari - MAELEZO
..................
Na: Frank Shija -
MAELEZO
Katika kuhakikisha
inaongeza nguvu katika usimamizi wa Mifumo yote ya Sekta za Umma iliyofanyiwa
maboresho PS3 imejipanga kuwajengea uwezo watumiaji wa mifumo hiyo katika eneo
la usimamizi ili ifanyekazi kwa ufanisi na kuwa endelevu hata mara baada ya Program hiyo kumaliza muda
wake ifikapo 2020.
Hayo yamebainishwa
leo na Mkuu wa Timu ya Fedha kutoka Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta
za Umma (PS3) Dkt. Gemini Mtei alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hizi
wakati wa mafunzo kwa ajili ya watumiaji wa Mfumo mpya wa Uandaaji wa Mipango
na Bajeti katika Serikali za Mitaa (PlanRep) Jijini Mbeya leo.
Dkt. Gemini amesema
kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufanya maboresho katika mifumo
mbalimbali iliyokuwa inatumika na Serikali na kuongeza kuwa jambo kubwa la
kutilia mkazo kwa sasa ni juu ya namna ambavyo mifumo hiyo itasimamiwa ili iwe
endelevu.
“Jambo ambalo sasa
tunatarajia kulitilia mkazo zaidi ni eneo la usimamizi wa mifumo ya sekta za
umma, tunataka kuona mifumo hii ikiendelea hata baada ya Programu yetu ya PS3
itakapomaliza muda wake,” alisema Dkt. Gemini.
Alisema kuwa kwa
kutambua umuhimu wa usimamizi wa mifumo PS3 iliona haja ya kuendelea na mifumo
iliyokuwepo badala ya kuja na mifumo mipya jambo ambalo limewezesha Serikali
kuendelea kuwa msimamizi wa karibu wa mifumo hiyo.
Akizungumzia mafunzo hayo ya Mfumo mpya wa Uandaaji wa
Mipango na Bajeti katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep), Dkt. Gemini
amesema kuwa mfumo huo ni matokeo ya changamoto zilizoanishwa na watumiaji
(wafanyakazi wa serikali) ambao walibainisha maeneo ambayo wangependa yafanyiwe
maboresho.
Alizitaja changamoto
hizo kuwa ni pamoja na matumizi makubwa ya rasilimali fedha itokanayo na mchakato
mzima wa uandaaji wa bajeti uanzia ngazi ya kijiji ambapo inahusisha rasilimali
watu ambao wote wanahitaji kugharamiwa.
Dkt. Gemini anesema
kuwa baada ya kuainishwa kwa changamoto hizo TAMISEMI walikuja na mapendekezo
ya kuufanyia maboresho mfumo huo ambao umekuja kutatua changamoto hizo ikiwemo
kupunguza gharama kwa kurahisha mawasiliano kwa njia ya Kielekroniki badala ya
mtu kufunga safari kutoka sehemu moja hadi nyingine, lakini pia kupitia mfumo
huo mtumiaji ataweza kufanya marekebisho ya Bajeti yake au taarifa yake bila ya
kuchapisha nakala yote jambo linaloondoa gharama.
Kwa upande wake
Mtaalamu wa Masuala ya Tehama kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI James Mtatifikolo
amesema kuwa Serikali kupitia OR – TAMISEMI ndiyo yenye dhamana ya kuisimamia
mifumo hiyo baada ya kujengewa uwezo na PS3.
Mtatifikolo aliongeza
kuwa maboresho hayo ya mifumo hasa wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti (PlanRep)
ni kwamujibu wa mahitaji ya Sera ya Tehama na miongozo mbalimbali ya Serikali.
Pamoja na kuwa mradi
wa huu PS3 unatekelezwa katika Mikoa 13 na Halmashauri 93 za Tanzania Bara bado
manufaa yake yanazifikia Halmashauri zote kupitia miradi mbalimbali
inayotekelezwa.
Katika muendelezo wa
kuwajengea uwezo watumiaji wa Mifumo iliyofanyiwa maboresho Serikali kwa
kushirikiana na USAID Tanzania/PS3 wanaendesha mafunzo ya nchi nzima ambapo
yanawashirikisha watumiaji wa mifumo ya PlanRep na Mfumo wa Fedha (FFARS)
ambapo washriki watano kutokoa Halmashauri 185 na wane kutoka mikoa yote ya
Tanzania Bara.





0 Comments