Kocha
wa Liverpool U18 Steven Gerrard amesema kuna umuhimu wa Livepool
kumsainisha mlinzi wa kati wa Southampton Virgil van Dijk ili kuweza
kuendana na kasi ya ushindani katika mashindano msimu huu.
Gerrard
alisema anahisi kuwa ili Jurgen Klopp aweze kufurahia msimu wa
mafanikio huko Liverpool anapaswa kumsajili beki huyo ambaye amekuwa na
kipaji kikubwa uwanjani na ambaye anajua nini anatakiwa kukifanya awapo
uwanjani.
Aliiambia BT Sport: "Ndio [yeye ni lazima].
"Kwa ajili yangu, ikiwa unataka kushindana katika ligi na katika Ligi ya Mabingwa (Van Dijk anahitajika).
"Timu ipo vizuri lakini bado tunahitaji saini mbili au tatu ndani."
0 Comments