Daktari ‘feki’ Abdallah Juma akiwa chini ya ulinzi wa Askari waliofika katika hospitali hiyo mara baada ya kupata taarifa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amana,Zainab Hoti akizungumza
waandishi habari juu wananchi kuacha njia ya mkato katika kupata huduma
katika hospitali ya Amana.picha na Emmanuel Massaka.
Daktari wa Kitengo cha Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi
(WAVIU) wa Hospitali ya Amana, Dkt. Shani Mwaruka akizungumza na
waandishi wa habari juu ya kumnasa Daktari ‘feki’ katika hospitali hiyo
leo jijini Dar es Salaam.
.........................................
Mkaazi wa jiji la Dar es Salaam, Abdallah Juma aliyewahi
kukamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akidaiwa kujifanya
daktari amenaswa tena katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa kufanya
kazi katika hospitali hiyo wakati sifa za udaktari hana. Juma amenaswa
leo ndani ya Hospitali ya Amana, majira ya mchana, akijifanya daktari,
baada ya kuwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo.
Kukamatwa
kwa Juma kunakuja ikiwa ni miezi mitatu tu imepita tokea Juni 19 mwaka
huu alipo kamatwa katika hospitali ya Muhimbili kwa kujifanya daktari.
Katika hospitali ya Muhimbili kijana huyo alijifanya kutoa huduma katika
maabara kuu huku uongozi ukiwa hauna taarifa ya kuwepo kwa huduma
aliyokuwa akiitoa kitu ambacho kilisababisha kushtukiwa na kukamatwa.
Baada
ya kukamatwa Uongozi wa hospitali hiyo ulifanya uchunguzi na kubaini
kuwa kijana huyo hakuwa daktari bali daktari feki kama alivyokuwa
akijitambulisha na kwamba amekamatwa mara baada ya kuwekewa mtego na
askari wa hospitali hiyo. Daktari wa Kitengo cha Watu wanaoishi na
Virusi vya Ukimwi (WAVIU), Shani Mwaruka alikiri kukamatwa kwa kwa
mtuhumiwa huyo.
Amesema, Juma alinaswa baada ya
uongozi kupata malalamiko kutoka kwa watu waliokuwa wakihitaji huduma
katika hospitalini hiyo. Amesema tayari hospitali hiyo iliweka mtego
imara wa maofisa wake, ambapo Juma aliingia bila hofu yeyote na kukutana
na watu ambao alitaka wampe fedha ili awahudumie ndipo aliponaswa.
Baadhi
ya watu waliodaiwa kuombwa fedha na daktari huyo feki, wamesema
aliahidi kuwatafutia kazi mbalimbali katika hospitali hiyo.
Nae
mwananchi aliyekwenda kupata huduma hospitali ya Amana Cecilia amesema
Agosti 9 mwaka huu, kijana huyo aliwaeleza kuwa kuna kazi katika
hospitali ya Amana na yeye kama daktari bingwa anayefanya kazi hapo
anaweza kuwasaidia.
“Alituambia kuwa fomu
zinatolewa katika hospitali ya muhimbili sh. 150,000 lakini kwakuwa wao
ni madakatari atatufanyia kwa sh. 100,000 tu. Tulichanga fedha hiyo na
ilifikia 800,000 tukampatia,”alieza Cecilia. Ameongeza,Juni 19 mwaka
huu aliwaita katika hospitali ya Amana ili kufanyiwa usahili lakini
hakutokea na simu akawa hapokei.
“Tuliamua
kuuliza kwa madakatari kama wanamfahamu lakini hakuna aliyemfahamu
ndipo tulipobaini kwamba tumetapeliwa na kuamua kufanya mtego kwa
kushirikiana na uongozi uliofanikisha kumnasa leo ,”alieleza.
0 Comments