Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Dar es salaam Kate Kamba
ameitaka idara ya ardhi wilaya ya Ilala kuhakikisha kuwa wanafanya kazi zao kwa
juhudi zaidi ili kuondoa tatizo la kutorasimishwa kwa maeneo mbalimbali hapa
nchini hasa miji inayokua ambayo baadae ianakuwa kero kwa wananchi.
Hayo
ameyasema jijini Dar es salaam Aprili
14, 2018 kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi ambayo ni utekelezaji wa ilani
ya uchaguzi wa chama Cha mapinduzi CCM katika kipindi Cha julai _Disemba 2017
kwenye sekta ya huduma za Jamii, Afya,
maji, ujenzi wa shule, miundombinu pamoja na uwezeshaji wananchi
kiuchumi.
Mkuu
wa wilaya ya Ilala Sophia mjema.
Aidha katika
ziara hiyo iliyowahusisha madiwani, viongozi wa CCM Ilala pamoja na wakuu wa
idara imetembelea miradi ya ujenzi wa shule za juhudi na uhuru mchanganyiko na
kisima cha maji cha kisukuru ambapo
amewataka madiwani kushirikia kikamulifu kwenye ujenzi wa miradi hiyo ili
kugundua mapungufu na kuyafanyia
marekebisho kwa haraka.
Mwenyekiti
CCM mkoa Bi. Kamba ameitaka halmashauri kuangalia jinsi ya kupunguza gharama za
ujenzi wa miradi na iwe katika hali ya ubora ikiwemo kuondoa gharama zisizo za
lazima kwa kutumia mafundi wa maeneo husika kwa bei nafuu pamoja na kununua
saruji zisizotozwa kodi.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Dar es salaam Bi.Kate Kamba (kushoto) akishauriana jambo pamoja na viongozi wengine wa chama hicho.
Sambamba na
hayo bi Kamba ameutaka pia uongozi wa wilaya ya Ilala kuangalia njia nzuri za
kuwasaidia vijana wanaoendesha bodaboda kufanya kazi zao kwa ufanisi bila
kuvunja sheria kwani wanategemewa kwenye utunzaji wa familia pamoja na
ukamataji unauzingatia utaratibu maalumu.
Kwa upande
wake Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia mjema amesisitiza kuwa wilaya ipo salama na
kuwakaribisha wawekezaji kuja kwa wingi na kuahidi kushirikiana nao kwa karibu
zaidi ili kukuza uchumi wa nchi na pale itakapogundulika uvunjifu wa amani
taarifa zitolewe ili wahusika wachukuliwe hatua.
mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Ilala Ubaya Chuma (katikati) akishauri jambo.
Naye
mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilala Ubaya Chuma amemshukuru mwenyekiti wa
mkoa kukubalia kutembekea miradi hiyo na
kumdhibitishia kuwa mahusiano yao na halmashauri yapo vizuri na mapungufu
yaliyojitokeza yatarekebishwa.
Hata hivyo
ameongeza kuwa kutokufikia malengo yaliyokusudiwa ni kutokana na upatikanaji
mdogo wa fedha kutoka serekalini pamoja
na kutofika kwa wakati hivyo kuomba usimamizi mzuri wa bajeti ili kupatikane
fedha za kutosha.



0 Comments