Kamanda wa Polisi mkoani mtwara Lucas Mkondya hivi karibuni akionyesha baadhi ya namba za pikipiki zilizokamatwa kwenye msako uliofanywa na jeshi hilo na kufanikiwa kukamata pikipiki kumi katika Kijiji cha Chikongo wilaya ya Tandahimba mkaoni hapa.
Kamanda wa Polisi mkoani mtwara Lucas Mkondya
hivi karibuni akionyesha baadhi ya vioo vya pikipiki zilizokamatwa kwenye msako
uliofanywa na jeshi hilo na kufanikiwa kukamata pikipiki kumi katika Kijiji cha
Chikongo wilaya ya Tandahimba mkaoni hapa.
Kamanda wa Polisi mkoani mtwara Lucas Mkondya
hivi karibuni akionyesha baadhi ya pikipiki zilizokamatwa kwenye msako
uliofanywa na jeshi hilo na kufanikiwa kukamata pikipiki kumi katika Kijiji cha
Chikongo wilaya ya Tandahimba mkaoni hapa.
Na.Martina Ngulumbi
JESHI la Polisi Mkoa wa Mtwara
linawashikilia watuhumiwa 46 katika matukio matatu tofauti ikiwemo wahamiaji
haramu 23, wizi wa pikipiki 13 na uchochezi kwa njia ya mitandao 13.
Akizungumzia matukio hayo hivi
karibuni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya amesema kuwa jeshi hilo
linawashikilia wahamiaji 23 kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria.
Amesema kuwa watuhumiwa hao walikutwa
katika eneo la Chikongola Wilaya ya Mtwara baada ya askari wa doria kupewa
taarifa na raia wema wanaoishi karibu na nyumba za wageni waliyofikia wageni
hao zao kihinga na lantumento.
Mkondya amesema kuwa wingi wa watu hao
uliwashtua watanzania wenye nia njema ambao walitoa taarifa kwa jeshi la polisi
ambapo baada ya ubekuzi ilibainika kuwa wapo watu 23 kutoka mataifa matatu
tofauti ambapo raia wa kongo 13, Rwanda 7 ma 2 kutoka Burundi.
Ambapo katika mahojiano ya awali
liliongesha kuwa wahamiaji hao walikuwa wakisafirishwa kwenda ufaransa kwa
kupitia visiwa vya Comoro.
Katika tukio lingine kamanda amesema
kuwa wanawashikilia watu 13 ambao wanajihusisha na mtandao wa wizi wa pikipiki
katika kijiji cha chikongo wilayani tandahimba.
Aidha jeshi hilo limebaini kuwa
mtandao umegawanyika katika makundi matatu ambapo kundi la kwanza ni wezi
wanaofanya wizi wa pikipiki maeneo mbalimbali kisha kuzipelekea kwa
wanaohifadhi na mwisho kwa wauzaji ambapo kundi hilo linaongozwa na Mohamed
Juma (simba).
Katika tukio lingine Jeshi la Polisi
linawashikilia wanafunzi 9 wa Chuo Kikuu cha Stella Maris Mtwara na Daktari wa
Hospitali ya Mission Nanyamba halmashauri ya mji Nanyamba.
Amesema kuwa watuhumiwa hao kwa
nyakati tofauti wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii ikiwemo ‘Watsapp’ na
Telegram’ kwa kumkashifu Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na
kuhamasisha maandamano yasiyo na kibali ya April 26 mwaka huu.
Jeshi la polis linatoa onyo kali kwa
watu kujiepusha kutumia mitandao ya kijamii vibaya na kupelekea
uvunjifu wa sheria za nchi ambapo katika matukio yote upelelezi bado
haujakamilika.



0 Comments