Random Posts

Matukio Katika Picha Wiki hii

 Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John, akimkabidhi  mshiriki kutoka Tunisia Bw. Jabali Belhanssen cheti cha ushiriki wa mafunzo ya utafiti ambayo yalifanyika jijini Dar es Salaam mwishonimwa wiki kwa ushirikiano wa Taasisi ya Usimamizi wa Kodi Afrika (ATAF) na Chuo cha Kodi (IAT). Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo, Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma na Utafiti Dr. Lewis Ishemoi na Mwakilishi ATAF Bw. Eugenio Bras.
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya biasahara ya CBA hapa nchini Dkt Gift Shoko, akizungumza na wateja wa mkoa wa mwanza kwenye hafla ya siku ya wateja wa benki hiyo ili kutambuana na kubadilishana mawazo, iliofanyika jijini Mwanza.Huduma ya M-Pawa inayotolewa na Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) imetoa mikopo yenye thamani ya Sh10 bilioni kwa wateja wake katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu.
 Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John akimkabidhi  mshiriki kutoka Tunisia Bw. Jabali Belhanssen cheti cha ushiriki wa mafunzo ya utafiti ambayo yafanyika jijini Dar es Salaam kwa ushirikiano wa Taasisi ya Usimamizi wa Kodi Afrika (ATAF) na Chuo cha Kodi (IAT). Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo, Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma na Utafiti Dr. Lewis Ishemoi na Mwakilishi ATAF Bw. Eugenio Bras.
Baadhi ya washiriki wa Warsha ya Mafunzo kwa Mtandao wa Watafiti wa Kodi Afrika (ATRN) waliosimama wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John (aliyekaa katikati) baada ya kufunga mafunzo hayo. Wengine kutoka kulia ni, Mwakilishi wa Taasisi ya Utafiti Barani Afrika (ATAF) Bw. Eugenio Bras, Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi Taaluma na Utafiti Dr. Lewis Ishemoi, Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo na Mkufunzi wa mafunzo hayo Prof. Nicaise Mede kutoka Benin.

Picha zote na Prona Mumwi-Mtazamo News

Post a Comment

0 Comments