Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, Fokas Bundala(wa
kushoto) akipanda mche wa mti wa asili aina ya mninga ,katika shule ya
msingi Visiga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti ya asili
inayofanywa na shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na
masuala ya upandaji miti la SAHO,(wa kulia) ni diwani kata ya Visiga
Mbegu Kambi Legeza (picha na Mwamvua Mwinyi)
Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala ya upandaji miti la SAHO,(wa kwanza kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake baada ya kupanda moja ya mche wa mti wa asili ,katika shule ya msingi Visiga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti ya asili inayofanywa na shirika hilo.(picha na Mwamvua Mwinyi
Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala ya upandaji miti la SAHO,(wa kwanza kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake baada ya kupanda moja ya mche wa mti wa asili ,katika shule ya msingi Visiga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti ya asili inayofanywa na shirika hilo.(picha na Mwamvua Mwinyi
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
JAMII
imehimizwa kupanda miti hasa ya asili ambayo ipo hatarini kutoweka
pamoja na kulinda mazingira kwa faida na manufaa ya kizazi kijacho.
Aidha wananchi wameaswa kuacha kukata miti na misitu ovyo kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha kuondoa uoto wa asili.
Rai
hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la -
SAHO-linalojishughulisha na masuala ya upandaji miti na kuhimiza kutunza
mazingira , Emmanuel Luamba wakati wa uzinduzi wao wa kampeni ya
upandaji miti kata ya Visiga ,Kibaha Mkoani Pwani.
Alisema
wananchi wanahimizwa kupanda miti lakini isisahaulike miti ya asili
ikiwemo mninga,mkwaju,mkongo ambayo ina faida zake katika kukuza uchumi
,kuleta hewa safi na kuwa na nchi ya kijani.
Luamba
alieleza wameotesha miche ya miti ya asili ipatayo 10,000 ambayo
wanaisambaza iweze kupandwa taasisi za umma ikiwemo mashuleni ,kwa
wananchi kata ya Visiga, kisha ngazi ya halmashauri na baadae Mkoa.
"Tumeanzia
taasisi za umma ikiwemo shule mbalimbali na jamii ili kuwa na uelewa wa
kujua faida za miti hii kwa manufaa ya sasa na vizazi vinavyokuja"
alielezea Luamba.
Akizungumzia ujio wa shirika hilo ,mwenyekiti huyo alibainisha wanatarajia kuwa na matawi nchi nzima .
Luamba
alielezea kwamba lengo lao ni kurejesha miti asili kwa kiasi kikubwa
kwamaana imekuwa ikivunwa kwa kasi na kuwa na hatari ya kutoweka .
Nae
diwani wa kata ya Visiga Mbegu Kambi Legeza aliwataka wananchi
kushirikiana na serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kupanda miti
na kuitunza.
"Ni jukumu letu sote kuunga mkono kampeni hii ili kuwa na maeneo na nchi ya kijani pamoja na hewa safi " alisema Legeza.
Legeza
alikemea ukataji miti kiholela na kuchoma moto miti kwa ajili ya mkaa
kusiko kwa utaratibu maalumu hali inayosababisha kupoteza miti .
Aliishukuru
SAHO kwa kuunga mkono juhudi za serikali kuhakikisha kunarejeshwa uoto
wa asili na kutunza na kupanda miti kwenye mazingira yanayotuzunguka.
Mgeni
rasmi katika uzinduzi huo ,makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa
Kibaha ,Fokas Bundala aliwataka wananchi kuilinda miche ya miti
wanayopewa kupanda badala ya kuitelekeza .
Kwa
upande wake ,mwanafunzi wa shule ya msingi Visiga ,anaesoma darasa la
saba ,Abdul Faraji alieleza wamepanda miche ya miti shuleni hapo na
alilishukuru Shirika hilo kwa kuona umuhimu kuanza na kampeni hiyo
katika shule mabalimbali ili kupata ufahamu wa miti hiyo.
Alisema
wamekuwa wakisikia miti ya asili bila kujua ni ipi na faida zake lakini
sasa atakuwa balozi mzuri kuwaelimisha watoto wengine juu ya suala hilo
.


0 Comments