Random Posts

Wanachama wa Chama Cha ACT Wazalendo Watakiwa Kuwa Chachu ya Kuchochea Maendeleo ya Watanzania.

Na Mwandishi Wetu

Katibu mkuu wa chama Cha ACT wazalendo Dorothy semu amewataka wanachama wa chama hicho kuwa wazalendo na chachu ya kuchochea maendeleo ya watanzania.

Hayo ameyasema jijini Dar es salaam wakati akipokea zaidi ya wanachama wapya 100 waliojiunga na chama hicho ambapo amewasisitiza kushirikiana pamoja na viongozi katika kujenga chama chenye ueledi na udhubutu wa kuhoji kwani ndio  viongozi wa kesho.
 Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha Act mkoa wa Dar es salaam Salumu Sudi amewataka wanachama hao kuanzisha matawi kwenye maeneo yao na kugombea nafasi mbalimbali zilizowazi ndani ya chama hicho.

Hata hivyo ameongeza kuwa wanatarajia kuanzisha ligi ya mpira wa miguu ya chama cha Act mwezi Mei mwaka huu ambayo itahusisha majimbo yote ya mkoa wa Dar es salaam ikilenga kuibua vipaji vya vijana pamoja na kukuza ushirikiano ndani ya jamii.

Post a Comment

0 Comments