Random Posts

Matukio Katika Picha Kutoka Bungeni Mjini Dodoma

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi ,Vijana Ajira,  na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiteta na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, Bungeni jijini Dodoma, Mei 16, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma, Mei 16, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri wa Kilimo na Mifugo, Luhaga Mpinda  akitoa maelezo kuhusu uhakika wa usalama wa nyama wanayokula watanzania, Bungeni jijini Dodoma, Mei 16, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu akizungumza na wanawake kutoka Mbeya  waliotembelea Bunge kwa mwaliko wa Naibu Waziri wa Kilimo Mary Mwanjelwa kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 16, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Dkt. Harrison Mwakyembe. Kulia ni Mbunge wa Lupa,  Bvictor Mwambalaswa na watano kulia ni Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mbunge wa Madaba, Mheshimiwa Joseph Mhagama kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 16, 2018. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Post a Comment

0 Comments