Mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo(aliyeinama) wakati alipotembelea maduka ya bidhaa ya mafuta ya
kupikia na sukari ,Loliondo ,Mailmoja ,Mjini Kibaha,(Wa pili kutoka
kulia) ni kamanda wa polisi wa mkoa huo , (ACP) Jonathan Shanna na wa
kwanza kushoto mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoani Pwani ,Abdallah
Ndauka.
(picha na Mwamvua Mwinyi).
Mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo
,wakati alipotembelea maduka ya bidhaa ya mafuta ya kupikia na sukari
,Loliondo ,Mailmoja ,Mjini Kibaha
(Picha zote na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
SERIKALI
mkoani Pwani,imewahakikishia wananchi kuwa inawasimamia wafanyabiashara
wa mafuta ya kupikia ,washushe bei ya bidhaa hiyo ambayo kwasasa
inauzwa lita moja sh.5,000 kutoka sh.3,200 iliyokuwa ikiuzwa kipindi cha
nyuma.
Aidha
imetoa onyo kwa wafanyabiashara wa sukari na mafuta hayo, ambao
watajaribu kuficha bidhaa hizo kwa lengo la kujitajirisha haraka haraka
baadae kwa kupandisha bei na kudai atakaefanya hivyo atakiona.
Mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo
aliyasema hayo wakati alipotembelea maduka ya bidhaa hizo ,Loliondo
,Mailmoja ,Mjini Kibaha huku akiwa ameambatana na kamanda wa polisi wa
mkoa huo , (ACP) Jonathan Shanna .
Alisema
Mei 16 mwaka huu,waliamua kutembelea baadhi ya magodauni na maduka ya
bidhaa hizo ambapo wamejiridhisha kwa kukuta sukari ikiuzwa bei nzuri na
maeneo mengine wakishusha madumu ya mafuta kwa ajili ya kuuzia walaji.
Ndikilo alieleza kwamba ,hategemei kuona wala kusikia kuna mfanyabiashara atakaefanya kitendo hicho ili bidhaa hizo ziwe adimu .
“Kama
yupo mfanyabishara atakaejaribu kuficha mafuta na sukari kwa uroho wa
fedha ,atakumbana na mkono wa sheria na hatutosita kumchukulia hatua za
kisheria”
“Serikali
inachunguza wote watakaoficha bidhaa hizo ,na jeshi la polisi mkoani
hapa chini ya kamanda Shanna linaendelea na misako mbalimbali na
kusimamia suala hili na wamejipanga”alisisitiza Ndikilo.
Akizungumzia
sukari ,Ndikilo ambae pia ni mkuu wa mkoa huo,alisema bidhaa hiyo
ilikuwa ikiuzwa 2,600 kwa kilo lakini imeshuka hadi 2,400/2,300 .
Mwenyekiti
wa wafanyabiashara mkoani Pwani, Abdallah Ndauka aliwataka
wafanyabiashara watoe huduma kama inavyostahili na kwa wakati.
Aliwaomba wazalishaji wa bidhaa viwanda kuzalisha na kusambaza kwa wingi bila kuwakwaza wananchi.
Ndauka
alisema kuwa,kama chama watawashughulikia wafanyabiashara
watakaokwamisha jambo hilo na kuwaasa wawe sehemu ya kutoa huduma
stahiki hasa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Nae
kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ,Shanna alisema wameyabeba maagizo
yaliyotolewa na kusema wanajua magodauni,store na maduka yote yanayouza
bidhaa hizo hivyo asithubutu mfanyabiashara kulijaribu jeshi hilo.
Shanna alielezea,ameshayapokea maelekezo kazi yake kubwa ni utekelezaji wa vitendo kwani wanaintelijensia ya kutosha.
Kwa
upande wao wafanyabiashara akiwemo Kassim Haji ,alisema mafuta ya
kupikia yalipotea lakini kwasasa kuanzia Mei 16 yameanza kuingia na kwa
yeye anatarajia kupokea madumu 600.
Alisema
wanatarajia kushusha bei baada ya kuanza kupelekewa mafuta kwani awali
kulikuwa na shida bandarini na anaahidi kushusha gharama ya bidhaa hiyo.
Nao
baadhi ya wananchi waliokuwepo soko la Loliondo kwa ajili ya
kujinunulia vyakula na bidhaa mbalimbali akiwemo Zulfa Rashid ,alisema
bidhaa inayowaumiza ni mafuta ya kupikia.
Aliomba
mafuta hayo yashushwe bei kwani yanauzwa kwa sh,5,000 kwa lita moja
fedha ambayo ni kubwa na maisha ni magumu hasa kuelekea kipindi cha
mwezi mtukufu wa Ramadhani.
“Tunaomba
gharama zishushwe ,serikali isimamie suala hilo,na tunashukuru mkuu wa
mkoa kuja kuzungumza na sisi ,pamoja na kutuhakikishia bidhaa hizo
zitashushwa bei.
Zulfa alisema, wengi wao wanatumia nazi na kuacha kununua mafuta kutokana na gharama kupanda tofauti na zamani.




0 Comments