Kivuko kipya cha MV. MWANZA chenye
uwezo wa kubeba tani 250, ambazo ni sawa na kubeba magari 36 na abiria
1,000 kwa wakati mmoja, kinachojengwa na kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine
Transport Boatyard ambacho kinagharimu jumla ya shilingi za kitanzania bilioni
8.9 fedha kutoka serikali ya Tanzania. Kitatoa huduma kati kigongo na Busisi
Mkoani Mwanza.
Kivuko kipya cha MV. MWANZA chenye
uwezo wa kubeba tani 250, ambazo ni sawa na kubeba magari 36 na abiria
1,000 kwa wakati mmoja, kinachojengwa na kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine
Transport Boatyard ambacho kinagharimu jumla ya shilingi za kitanzania bilioni
8.9 fedha kutoka serikali ya Tanzania. Kitatoa huduma kati kigongo na Busisi
Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TEMESA Brigedia
Jenerali Mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri, akipanda ngazi kukagua ujenzi wa
kivuko kipya cha MV. MWANZA, nyuma yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Songoro Marine Transaport Boat Yard Ltd (inayojenga kivuko hicho) Salehe
Songoro, akifuatiwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme( TEMESA) Dkt.
Mussa Iddi Mgwatu.
Mtendaji Mkuu
wa Wakala wa Ufundi na Umeme( TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (wa kwanza kulia)
akiongea na waandishi wa habari baada ya ukaguzi wa kivuko kipya cha MV. MWANZA
kulia kwake mwenye miwani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TEMESA Brigedia
Jenerali Mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri.
Picha na Kitengo cha Habri na Mawasiliano TEMESA
Na.
Theresia Mwami - TEMESA
Serikali kupitia Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA), imeahidi kukamilika kwa ujenzi kivuko kipya cha
Kigongo Busisi (MV. MWANZA) unaofanywa kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport
Boatyard ifikapo mwezi Juni 2018. Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa
kubeba tani 250, ambazo ni sawa na kubeba magari 36 na abiria 1,000 kwa wakati
mmoja.
Akizungumza na waandishi wa
habari, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa kivuko hicho, uliofanywa na baadhi ya
wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TEMESA mapema leo, Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt.
Mussa Iddi Mgwatu alisema ujenzi huo unagharimu jumla ya shilingi za kitanzania
bilioni 8.9 na ulianza rasmi tarehe 28/08/2017 na kwamba tayari umekamilika kwa
asilimia 95.
“Namuagiza Mkandarasi
kuhakikisha kuwa ujenzi wa kivuko hiki unakamilika kwa aslimia 100 ifikapo
mwezi Juni,2018 kama ilivyoainishwa kwenye mkataba ili kuweza kuboresha zaidi huduma
ya uvushaji abiria na mizigo yao katika eneo Kigongo – Busisi”, aliongeza Dkt.
Mgwatu.
Aliongeza kuwa kukamilika kwa
ujenzi wa kivuko cha MV. MWANZA kutafanya eneo la Kigongo Busisi kuboresha zaidi
huduma za uvushaji kwani kwa sasa tayari kuna Kivuko cha MV. Misungwi ambacho
pia kina tani 250, MV. Sengerema tani 170 na MV. Sabasaba tani 85.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Bodi ya ushauri ya TEMESA Brigedia Jenerali
Mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri
alisema kuwa, serikali inalengo la kuboresha hali ya maisha ya wananchi, kwa kuwawekea
miundombinu salama ya vivuko, ili kuhakikisha wanapata huduma bora na salama
wakati wote.
Aliongeza kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutatoa nafasi ya
ukarabati mkubwa wa vivuko vingine vinavyotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi
kufanyika kwa awamu. Aidha alitumia
nafasi hiyo pia kuwapongeza TEMESA kwa kazi nzuri ya usimamizi wa ujenzi wa
kivuko hicho, kwa kuhakikisha kuwa unakamilika kwa wakati kama ilivyo kwenye
mkataba wa ujenzi wake.
Nae Mkurugenzi
Kampuni ya Songoro Marine Transaport Boat Yard Ltd, Major Songoro, aliishukuru
Serikali kwa kuendelea kuiamini kampuni hiyo na kuahidi kuimaliza kazi hiyo kwa
haraka na ustadi mkubwa.
0 Comments