Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa Michezo
akichangia hoja kuhusu Muswada wa Sheria ya upatikanaji wa Taarifa ya mwaka
2016 ambapo alisema Muswada huu utasaidia kuongeza uwazi na uwajibikaji pia
utasaidia kukuza tasnia ya habari nchini, Wakati wa Kikao cha 2 leo Bungeni
Mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye
Ulemavu) akichangia akichangia hoja kuhusu Muswada wa Sheria ya upatikanaji wa
Taarifa ya mwaka 2016 ambapo alisema Muswada huu utasaidia kukidhi hitaji la
kikatiba la watu kupata taarifa, Wakati wa Kikao cha 2 leo Bungeni Mjini
Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju
akichangia hoja kuhusu Muswada wa Sheria ya upatikanaji wa Taarifa ya mwaka
2016 ambapo alisema na kusisitiza umuhimu wa muswada huu ikiwemo kuongeza wigo
wa upatikanaji wa taarifa kwa waandishi wa habari.
Waziri
wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akijibu hoja zilizotolewa na
wabunge kuhusu Muswada wa Sheria ya upatikanaji wa Taarifa ya mwaka 2016 ambapo
aliwataka wabunge kuacha kupotosha kuwa muswada huu utavibana vyombo vya habari
na kuwataka kuusoma na kuuelewa muswada huo
PICHA
NA HASSAN SILAYO-MAELEZO




0 Comments