Wanafunzi wa shule ya Msingi Mahembe Manispaa ya Singida wakifanya mitihani ya kumaliza elimu ya Msingi.
.....................................................................
Na Mwandishi wetu-Singida
Wanafunzi elfu 21, 417 wa shule za Msingi 514
katika halmashauri saba za Mkoa wa Singida leo wameanza mitihani ya kumaliza
elimu ya msingi inayofanyika nchini kote.
Wanafunzi hao mabao wavulana ni elfu
9,639 wasichana ni elfu 11,778 wamefanya mitihani ya masomo ya
kiswahili, hisabati na sayansi kwa siku ya leo huku wakimalizia na
masomo ya kiingereza na maarifa ya jamii.
Afisa Elimu Mkoa wa Singida Florian
Kimolo amesema mitihani inafanyika kwa amani na utulkivu kutokana na
kufanya maadalizi mapema kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa na halmashauri zote za Mkoa wa Singida.
Kimolo ameongeza kuwa Mkoa ulitoa semina
nelekezi kwa waalimu wasimamizi 2158 ambao wanasimamia mitihani katika
shule 511 zenye wanafunzi wanaofanya mitihani hiyo ikiwa shule za
serikali ni 504 na za binafsi 7.
Amesema kuwa wanafunzi wasioona
wanaofanya mitihani ni 8 wavulana watano na wasichana watatu huku wenye
uoni hafifu ni 49 wavulana wakiwa 23 na wasichana 26.
Akiongea baada ya kuanza kwa mitihani
katika shule ya Msingi Mahembe iliyopo Manispaa ya Singida Mwalimu Mkuu
wa Shule hiyo Bwana Patrick Masong amesema mitihani inafanyika kwa
utulivu na watahiniwa wote wamehudhuria.
Masong amesema hakuna matatizo yoyote
yaliyojitokeza tangu waanze mitihani na wana imani zoezi hilo
litakamilika kwa usalama huku akisema ufaulu utakuwa mzuri kutoka na
walimu kuwafundisha vizuri wanafunzi hao.


