Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Kingani kata ya Kisutu, Method Kunambi akizungumza na wazazi wa wanafunzi shuleni hapo kuhusu changamoto zinazowakabili.
(Na Mwamvua Mwinyi)
........................................................................................
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
WAZAZI wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kingani,kata ya Kisutu,Bagamoyo,wamekubaliana kuchangia sh.40,000 kila mmoja ili kupata mil.60 zitakazowezesha kujenga hostel mbili za wanafunzi wa kiume.
Uamuzi huo utasaidia kupunguza tatizo la utoro na zero(O) wanazopata wanafunzi hao kwenye mitahani ya kumaliza kidato cha nne.
Wakizungumzia makubaliano hayo,akiwemo Charles Mngweno na Mary Dalu,walisema matokeo ya ufaulu ya kidato cha nne mwaka 2015 kwa upande wa wavulana hayaridhishi .
Mngweno alieleza kuwa tatizo kubwa ni kukosa hostel kwa wanafunzi hao na masuala ya utandawazi ndio yanayosababisha kufeli.
“Watoto wetu hawa siku hizi wanaendekeza kubet ligi za mipira ya ulaya,kucheza pool,kuchat na kwa upande wa shule ni kukosa hostel”alisema.
Nae Mary alifafanua kwamba wanafunzi wa kiume wapo 220 lakini hakuna anaekaa shuleni hivyo wanakumbana na mambo mengi mitaani na wakati wakienda na kurudi shuleni.
Aidha wazazi hao walisema ili kuunga mkono jitihada za serikali kutatua changamoto za kielimu watakuwa wanachangia boksi moja la karatasi nyeupe(lim paper) kwa ajili ya kuchapisha mitihani ya wiki .
Mwalimu wa taaluma shuleni hapo,Ibrahim Ndwata,alisema utoro na ukosefu wa hostel kwa wanafunzi wavulana kunachangia kupata O.
Ndwata alibainisha ,matokeo ya kidato cha nne mwaka jana,div I ilikuwa moja,div II ni sita,div III wanafunzi 11,div IV ni 49 na O ni 75.
mwenyekiti wa kamati ya ujenzi huo,Hassan Mbegu Mohammed,alisema wazazi hao watatakiwa kuchangia 20,000 katika awamu ya kwanza hadi ifikapo mwezi may mwaka huu.
Alisema awamu ya pili watamalizia kuanzia mwezi july ambapo wanatarajia ujenzi huo uanze mwezi june.
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Kingani,Method Kunambi,akizungumza katika kikao hicho kilichokuwa kikijadili maendeleo na changamoto zinazoikabili shule hiyo,alisema hostel zinasaidia kuinua taaluma.
Kwasasa wanafunzi wa kike shuleni hapo wanafaulu vizuri kuliko wavulana kutokana na kuwa na hostel mbili hivyo kupata muda wa kujisomea na kukaa chini ya uangalizi.
Mwalimu Kunambi alifafanua,hostel hizo zilijengwa kwa ushirikiano baina ya action aid Tanzania na halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kwa gharama ya sh.mil 400.
Alisema licha ya kuwa na mabweni hayo lakini bado yanahitajika manne ili kutosheleza wanafunzi wote wa kike waliopo.
Mwalimu Kunambi aliwaomba wazazi na walezi kuwa na malezi mema kwa watoto wao kwa kushirikiana na walimu pasipo kuwadekeza hali inayosababisha kushuka kitaaluma,mimba na utoro.
Mwenyekiti wa kikao hicho,alhaj Abdul Sharif alisema maendeleo ya sekta ya elimu yataletwa na wazazi,jamii pasipo kutegemea serikali pekee.
Kikao hicho kiliazimia kuchagua kamati ya taaluma itakayokuwa ikishughulikia changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo.
Waliochaguliwa kwenye kamati hiyo ni wazazi watano akiwemo Timothy Kasaini(Mwenyekiti),Mary Dalu(katibu),Kissina Shaban,Fatuma Ally na Jafari Ngogi.
No comments:
Post a Comment