Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaambia washtakiwa sita
wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya meno ya tembo akiwemo
mfanyabiashara Yusuf Yusuf (34) maarufu ‘Mpemba’, kuelekeza lawama zao
juu ya upelelezi kuchelewa kukamilika kwa mawakili wanaowatetea siyo wa
Serikali tu.
Hakimu Mkazi
Mkuu, Thomas Simba amesema hayo mapema leo asubuhi wakati kesi hiyo ya
uhujumu uchumi ilipofika kwa ajili ya kutajwa ambapo Wakili Wa serikali
alidai jalada.
Wakili Wa
Serikali Elia Athanas alidai kuwa taarifa walizopeleka Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam ambazo awali zilikosewa, walizifanyia marekebisho
lakini bado hazijarudishwa ili waweze kuwasomea washtakiwa maelezo ya
mashahidi (Committal.)
Hata
hivyo, washtakiwa wamelalamika na kudai kuwa kila wakija wanaambiwa
jalada halipo, ndipo hakimu akawashauri wawalalamikie pia mawakili
wanaowatetea na siyo wa upande wa serikali tu kwani na wao wamekuwa
wakikaa kimya tu.
"Muwe mnawalalamikia na mawakili wenu pia siyo wa Serikali tu, ili hii kesi iweze kwenda kwa haraka", amesema Simba
Kesi hiyo imahirishwa hadi Octoba 10 kwa ajili ya kutajwa
Mbali
na mpemba, washtakiwa ni Charles Mrutu (37) mkazi wa Mlimba, Morogoro,
Benedict Kungwa (40) mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima (30) mkazi
wa Mbezi, Ahmed Nyagongo (33) dereva na Pius Kulagwa (46)
Wote wanakabiliwa na mashitaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 785.6.
No comments:
Post a Comment